Ndege mpya ya Tanzania yenye uwezo wa kubeba abiria 262 yawasili

Ni furaha na vifijo kwa Watanzania baada ya kushuhudia ndege mpya ikitua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalim Julius Nyerere ambapo Rais Magufuli alipokea ndege hiyo mali ya Tanzania aina ya Boeng 787-8 Dreamliner inayobeba abiria 262.

Akiongea na Wananchi waliojitokeza uwanjani hapo, Rais anasema ndege nyingine tatu aina ya bombadier zitafika nchini Desemba mwaka huu.

Rais anasema mafanikio haya ni matokeo ya uchapaji kazi wa watanzania wote ambapo amewapongeza watanzania wote na kuwaomba walipe kodi ili kuweza kununua ndege zingine zaidi.

Rais amesema sababu za kuamua kulifufua shirika la ndege la Tanzania ni kurahisisha mawasiliano na usafiri na kuondoa aibu ya nchi yetu ambayo ina rasilimali nyingi na vivutio vingi lakini havimnufaishi mwananchi wa kawaida.

“Usafiri wa uhakika wa ndege utawezesha wananchi kufikia kirahisi masoko yaliyopo nje ya nchi ikiwemo kuuza samaki nje ya nchi, maua yaliopo arusha na mbeya, pia lengo lingine ni kupunguza gharama za usafiri wa anga,” alisema Rais Magufuli.

Pia alisema lengo lingine la kufufua shirika letu la ndege ni kupanua wigo kwenye sekta ya utalii nchini ambapo sekta hiyo haituingizii fedha za kutosha za kigeni kwa sababu ya kukosekana usafiri wa uhakika

Rais anaelezea miradi mbalimbali ambayo serikali inatekeleza ikiwamo kujenga madaraja ya juu nchini hususan katika jiji la Dar es salaam ili kurahisisha usafiri wa jiji hilo pamoja na mradi mkubwa wa umeme nchini Stiglers Gorge.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW