Habari

Ndege ya kijeshi ya Chile yatoweka na watu 38

Ndege ya kijeshi iliokuwa na abiria 38 imetoweka ikielekea Antarctica, kulingana na taarifa ya jeshi la wanahanga wa Chile.

Ndege hiyo kwa jina C-130 Hercules ilitoweka mwendo wa saa kumi na mbili muda wa Chile baada ya kupaa kutoka mji wa Kusini wa Punta Arenas.

Miongoni mwa waliotoweka na ndege hiyo ni wafanyakazi 17 na abiria 21 ambao walikuwa wakisafiri ili kutoa usaidizi wa kimipango.

Wanahanga wa Chile wamesema kwamba operesheni ya usakaji na uokoaji inaendelea ili kuiokoa ndege hiyo pamoja na abiria wake.

Kitengo cha habari cha EFE kimeripoti kwamba watatu kati ya abiria hao ni raia.

Rais wa Chile Sebastian Pinera amesema katika ujumbe wa Twitter kwamba amefadhaishwa na kutoweka kwa ndege hiyo na kwamba anachunguza hali katika kambi ya wanahanga ya Cerrillos katika mji mkuu wa Santiago

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Jenerali wa jeshi la wanahewa nchini Chile Eduardo Mosqueira aliambia chombo cha habari kwamba ndege hiyo haikuonyesha ishara zozote za kukabiliwa na tatizo kabla ya kutoweka.

Amesema kwamba ndege hiyo hueda ililazimika kutua baada ya kukabiliwa na upungufu wa mafuta katika safari yake ya kuelekea katika kambi ya rais wa Chile Eduardo Frei Montalya katika kiswa cha King George.

Ndege mbili za kivita aina ya F- 16 na meli nne zimeenda kusaidia katika usakaji wa ndege hiyo.

Katika taarifa nyengine , aliongezea kwamba kamouni zote za ndege zilizopo katika eneo hilo zitasaidia katika usakaji wa ndege hiyo.

Alisema kwamba rubani wa ndege hiyo alikuwa na uzoefu mkubwa na huenda alilazimika kutua baada ya mafuta kuisha.

Wanahewa wa taifa hilo wamesema kwamba ndege hiyo ilikuwa imefika maili 450 kati ya 770 ya safari yake wakati ilipopoteza mawasiliano ilipopitia katika eneo moja la maji linalounganisha eneo la Kusini mwa Atlantic na kusini mwa Pacific na linajulikana kwa hali mbaya ya hewa.

Lakini wanahanga wa Chile wanasema kwamba hali ya hewa ilikuwa shwari wakati ndege hiyo ilipotoweka.

Chile inadhibiti kilomita milioni 1.2 mraba wa eneo la Antarctic ikipakana na ardhi inayodaiwa kumilikiwa na UK na Argentina.

Katika eneo hilo inamiliki kambi tisa za kijeshi ikiwa ni nyingi zaidi ya taifa lolote lile duniani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents