AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Ndege ya pili mpya imewasili leo, uzinduzi kufanyika kesho

Ndege ya pili kati ya 2 zilizonunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewasili leo mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere (JNIA).

n5
Ndege ya pili ilivyo wasili leo ikipata saluti ya maji

Ndege hizo aina ya Dash 8 Q400 zilizotengenezwa na kiwanda cha Bombardier nchini Canada zinatarajiwa kuzinduliwa kesho kuanzia majira ya saa 2.00 asubuhi katika uwanja wa JNIA (Terminal 1).

n6

Katibu Mkuu wa (Uchukuzi) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk. Leonard Chamuriho amesema Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa ndege hizo.

Aidha, ndege ya kwanza iliwasili Septemba 20,2016. Ndege hizo zina uwezo wa kubeba abiria 76 kwa kila moja ambazo zitahudumia soko la ndani na nchi jirani.

Related Articles

Check Also

Close
Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW