Habari

Ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) yatua kwa dharura mjini Athens, Ugiriki baada ya kutokea ishara ya tahadhari ya moto sehemu ya mizigo!

Ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways iliyokuwa ikitokea Amsterdam ikielekea Nairobi, imelazimika kutua kwa dharura mjini Athens, Ugiriki baada ya kujitokeza ishara ya tahadhari ya moto sehemu ya mizigo.

KQ

Taarifa iliyoripotiwa mchana wa leo (July 6) na mtandao wa Standard Digital imesema ndege hiyo yenye namba KQ 117 iliyokuwa na jumla ya abiria 301, ilitua salama katika uwanja wa Athens kisha abiria wote na wafanyakazi wa ndege kupelekwa hotelini kwaajili ya kupisha uchunguzi wa chanzo cha ishara ya tahadhari ya moto katika eneo la mizigo la ndege hiyo.

Taarifa hiyo imeendelea kusema uchunguzi katika kifaa cha kugundua dalili za moto ulifanyika ili kubaini chanzo, lakini hakuna tatizo lolote lililoonekana.

Baada ya ukaguzi huo abiria walikuwa wanategemewa kuondoka Athens kuendelea na safari ya Nairobi majira ya saa 11 jioni ya leo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents