Michezo

Ndemla atua salama Sweden

Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kuwa kiungo wake, Said Hamisi Juma Ndemla amewasili salama Sweden tayari kuanza  kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini humo.

“Said Ndemla amewasili salama nchini Sweden tayari kuanza majaribio yake katika klabu ya AFC Eskilstima inayoshiriki ligi kuu nchini humo.” Imesema klabu ya Simba.

Safari ya Ndemla Sweden yaota mbawa

Ndemla alipaswa kuondoka Novemba 7 kwenda Sweden kwaajili ya kufanya majaribio  katika klabu ya AFC Eskilstuna lakini safari yake ilisogezwa mbele kwa siku mbili hadi tarehe 9 ya mwezi huu.

Simba SC yatoa baraka zote kwa Ndemla kutua Sweden

Ndemla atakuwa huko kwa takribani siku 14 kabla ya kurejea nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents