Burudani

Ndoa ya Barnaba na mchumba wake yanukia

Mchumba wa Barnaba, Zubeda amesema anafurahia maisha yake na mpenzi wake Barnaba na kwamba watafunga ndoa hivi karibuni.

bb-4

Zubeda ameiambia Bongo5 kuwa mipango ya ndoa imekamilika na kwamba wanasubiri kuamua tarehe tu.

“Tayari ameshatoa pesa ya barua pamoja na mahari, kwahiyo bado tu kupanga tarehe ya ndoa,” amesema Mama Steve. “Barua alitoa toka mwaka jana na pesa ya mahari ametoa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana japokuwa bado haijafika lakini najisikia furaha sana na naomba Mungu ifikie siku yenyewe nitajisikia furaha zaidi ya hapo nitakapofunga ndoa. Unajua kutolewa pesa ya barua na mahari na nilishavishwa pete ya uchumba siku ya birthday kwahiyo ninachokisubiria kwa hamu ni ndoa tu.”

Hata hivyo licha ya kusubira ndoa hiyo kwa hamu amekiri kuwa na changamoto nyingi ndani ya mahusiano yao.

“Kuna challenge nyingi sana, unaweza ukaamka asubuhi ukakuta simu inaita ukipokea simu unasikia baby, message za mapenzi, lakini mwanzo vilikuwa vinaniuza sana kwakuwa nilikuwa sivijui lakini kadri siku zivyonaenda nikawa ninazoea. Mpaka leo hii unasikia natarajia kufunga ndoa ujue nimepambana vya kutosha kutetea ndoa yangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents