Burudani

Ndoa ya Kevin Hart chupuchupu kuvunjika

Baada ya kukiri kuchepuka  siku chache zilizopita swali ni Je? Ndoa ya muigizaji Kevin Hart na mkewe Eniko ipo salama kweli?

Hilo ndiyo litakuwa swali la watu wengi ila majibu ni kwamba  ndoa hiyo imeponea katika tundu la sindano,  kwani wawili hao wameonekana wakikatiza mitaa ya Los Angeles -Marekani huku wakionyesha kuyasahau yaliyopita.

Kevin ambaye alikuwa mjini Atlanta siku ya jumatatu katika utengenezaji wa filamu mpya, ameonyesha kutokuwa na wasiwasi juu ya ndoa wake. Hata hivyo inadaiwa kuwa msanii huyo tayari ameshaongea na polisi kwa ajili ya kudhibiti video iliyopangwa kuachiwa na mwanamke aliyechepuka naye isisweze kuvuja.

Mke wa muigizaji huyo ambaye ni mjamzito amenaswa na kamera za mtandao wa TMZ, akiwa bado amevaa pete yake ya ndoa. Muigizaji huyo amewahi kumsaliti mke wake wa zamani aitwae Torrei Hart na kupelekea ndoa yao kuvunjika kabla ya kumuoa Eniko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents