Habari

Ndoa ya Morgan Tsvangirai yazua mambo, mchumba aliyemwacha ataka waziri huyo mkuu akamatwe


Drama ya mahakama inayomzunguka waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai aliyefunga ndoa na mchumba wake Elizabeth Macheka imefikia bapaya juzi baada ya aliyekuwa mchumba wake wa zamani Locardia Karimatsenga Tembo kutaka waziri huyo mkuu akamatwe.

Mwanasheria Jonathan Samukange anadai kuwa Tsvangirai alidanganya kwamba hakuwahi kumuoa Karimatsenga chini ya sheria za kitamaduni.

Mchumba wa zamani wa Tsvangirai, Locardia Karimatsenga

Wanasheria wake wanapanga kukutana na mwanasheria mkuu Johannes Tomana kufuatilia barua yao waliyomwandikia wakitaka kukamatwa kwa Tsvangirai.

Licha ya Tsvangirai kumwacha Karimatsenga November mwaka jana, anadai kuwa bado ni mke wake halali.

Ijumaa iliyopita mahakama iliamuru Tsvangirai asifunge ndoa kwakuwa alimwacha mchumba wake wa zamani anayedai walioona kimila na alimtolea mahari.

Waziri huyo mkuu wa Zimbabwe alifunga ndoa Jumamosi iliyopita na kudai kuwa alikuwa na uhusiano na wanawake kadhaa lakini sasa amempata ampendaye kwa dhati.

“I love this woman because I chose her myself. I will love her till the day I die,” aliwaambia wafuasi wake kwenye sherehe hiyo.

“I saw a beautiful woman,” he said. “I said she is beautiful for someone like me who has an eye for beautiful women.”

Tsvangirai amezipuuzia propaganda za chombo cha habari cha serikali kuwa maisha yake binafsi hayajatulia na hivyo kumfanya asiwezi kuiongoza nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents