Michezo

Ndoto ya Samatta kutimia leo, Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya UEFA, Aweka ujumbe huu

Ndoto ya Samatta kutimia leo, Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya UEFA, Aweka ujumbe huu

Ndoto ya Watanzania kuona raia wa kwanza wa taifa hilo kucheza kwenye makundi ya michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya (Champions League) inaweza isitimie hii leo. Mshambuliaji na nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta kupitia klabu yake ya Genk ya Ubelgiji amefanikiwa kufuzu kutinga hatua ya makundi, lakini hii leo anaweza kuukosa mchezo wa kwanza kutokana na majeraha aliyoyapata hivi karibuni.

Mabingwa wa Ubelgiji Genk watasafiri mpaka Austira kuvaana na mabingwa wa nchi hiyo klabu ya Salzburg katika uga wa Red Bull arena usiku wa leo.

Jumapili ya Septemba 8, Samatta alikuwa akiiongoza Tanzania kwenye mchezo dhidi ya Burundi wa kufuzu makundi ya kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia.

Japo Tanzania ilishinda mchezo huo kwa mikwaju ya penati, Samatta alipata majeraha ya goti.

https://www.instagram.com/p/B2Q1dCGIKq1/?utm_source=ig_embed

Mara tu baada ya kurudi Ubelgiji alienda kufanya vipimo na kubainisha kupitia ukurasa wake wa mtandao kijamii wa Instagram kuwa hakupata majeraha makubwa japo ametakiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda.

Hata hivyo hakubainisha ni kwa muda gani atasalia nje ya uwanja.

Ijumaa wiki iliyopita, KRC Genk iliingia uwanjani dhidi ya Charleroi kwenye ligi ya Ubelgiji. Samatta ambaye ni mshambuliaji tegemezi wa Genk hakucheza mchezo huo na wala hakuwepo kwenye benchi la wachezaji wa akiba. Genk ilipoteza mchezo huo kwa magoli 2-1.

samattaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Hata hivyo taarifa za kutia matumaini ni kuwa Samatta tayari anafanya mazoezi, na siku mbili zilizopita ametuma video kupitia ukurasa wake wa Instagram akipanda kilima kwa kasi.

Taarifa rasmi ya majina ya wachezaji watakaocheza katika mchuano huo wa leo usiku bado haijatolewa, na itakapotolewa ndipo Watanzania watahakikisha kama Samatta atashuka dimbani leo ama watasubiri mchezo ujao kumuona ndani ya Champions League.

Genk na Salzburg wapo Kundi E pamoja na mabingwa Liverpool kutoka England pamoja na Napoli kutoka Italia.

Takwimu zinaifanya Genk kuwa ndiyo timu isiyopewa kipaumbele kabisa kwenye kundi hilo. Timu hiyo licha ya kushiriki mashindano hayo mara mbili msimu wa 2002-03 na 2011-12 haikuweza kupata walau ushindi hata katika mechi moja kati ya 12 ilizocheza.

Katika misimu yote miwili Genk ilimaliza mkiani kwenye makundi iliyopangiwa.

https://www.instagram.com/p/B2ZkUwKIwNB/?utm_source=ig_embed

Ikifanikiwa kupata ushindi leo ama katika mechi zifuatazo watakuwa wamejiandikia historia mpya.

Kiuhalisia mchezo wa leo ndio utakuwa ‘rahisi’ kwa Genk, na kibarua dhidi yao kitakuwa kigumu watakapovaana na Liverpool na Napoli.

Michezo ya leo ya Champions League

Ukiachana na Salzburg dhidi ya Genk klabu nyengine zitakazochuana usiku wa leo ni:

Napoli vs Liverpool

B Dortmund vs Barcelona

Chelsea vs Valencia

Inter Milan vs Slavia Prague

Lyon vs Zenit St Petersburg

Benfica vs RB Leipzig

Ajax vs Lille

Credit by BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents