Michezo

‘Ndoto zangu kubwa ni kutwaa Premier League zaidi kuliko hata Champions League’ – Olivier Giroud 

Mchezaji wa Chelsea, Olivier Giroud amesema kuwa hajakata tamaa ya kutwaa taji la ligi kuu nchini Uingereza kwakuwa ndiyo ndoto zake kubwa kwa sasa.

The 32-year-old failed to lift the league title during his six years as an Arsenal player

Giroud raia wa Ufaransa amejiunga na ‘the Blues’  dirisha la usajili la mwezi Januari na tayari ameshatwaa taji la FA Cup.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32, ameiyambia The Guardian kuwa ndoto zake kubwa ni kuona nafanikiwa kutwaa kombe la Premier League zaidi kuliko hata Champions League kwakuwa anafahamu ugumu uliyopo wa kunyakuwa taji hilo.

Olivier Giroud admits his last dream in professional football is to win the Premier League

”Kushinda Premier League ndiyo ndoto zangu kubwa kama mchezaji pengine kuliko hata kutwaa Champions League, kwasababu nafahamu kunaugumu wa kiasi gani kushinda ligi hii,” amesema Giroud.

Olivier Giroud  ambaye amefanikiwa kunyakuwa kombe la ubingwa wa dunia mwaka huu nchini Urusi akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa ameongeza ”Nina wachezaji wenzangu hapa ambao wameshashinda kombe hili la Premier League, hivyo nawaonea wivu nahitaji na mimi nafanikiwa katika hilo.”

”Unaweza kuona tumepoteza na Wolves lakini tumemfunga Manchester City, hivyo ni ngumu sana kwa mimi kukata tamaa na ndoto yangu.”

Giroud ametuwa Stamford Bridge kwa dau la pauni milioni 18 mwezi Januari baada ya kuitumikia  Arsenal kwa miaka sita pasipokufanikiwa kutwaa kombe hilo la ligi.

Tangu atuwe Chelsea Mfaransa huyo anajumla ya magoli 10 kwenye michezo 36 aliyocheza huku akifanikiwa kufunga moja kati ya bao zuri kwa njia ya free-kick walipotoka sare ya mabao 2-2 kwenye michuano ya Europa League siku ya Jumamosi dhidi ya Vidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents