Michezo

Ndugu wa familia moja Makambako washinda bajaji za SportPesa

Shinda na SportPesa imeendelea kuchanja mbuga na mpaka sasa tayari bajaji 24 aina ya TVS KING zimeshapata washindi kutoka kila kona ya Tanzania huku zikiwa zimebaki bajaji 76 zinazoshindaniwa.

Siku ya Ijumaa, Novemba 17, timu ya SportPesa ilitua Makambako Iringa kwa ajili kukabidhi bajaji mbili za TVS KING kwa washindi wawili, Juviniki Edward Msambule (21) na Yusuph Ramadhani (28) ambao wote ni mafundi ujenzi.

Moja ya mambo ya kusisimua ni kwamba Juviniki na Yusuph ambao walikuwa washindi wa droo ya 18 na 19 ni ndugu wa familia moja ambao wamechangia mama na walishinda bajaji katika siku mbili zinazofuatana (Novembe 12 na 13).

Ndugu hao wa damu walikabidhiwa bajaji zao na Mkuu wa Wilaya na Njombe Bi Ruth Msafiri eneo la stendi ya mabasi, Makambako na baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Yusuph ambaye ndiye kaka mkubwa alitoa simulizi nzima ya maisha yao na jinsi bajaji hizo zitakavyoweza kubadili maisha yao.

SP: Mnatoka kwenye familia ya watu wangapi na wazazi wenu wanajishughulisha na nini?

Yusuph: Sisi kwa mama tumezaliwa watatu, yupo kaka yetu mkubwa, kisha nafuata mimi halafu Juviniki ni wa mwisho. Wazazi wetu ni wakulima wa kawaida lakini sisi watoto ndio wenye jukumu kubwa la kuwatunza kwasababu umri umewatupa mkono.

SP: Wewe binafsi una familia?

Yusuph: Ndio; nina mke na watoto wawili ambapo mtoto wa kwanza ana miaka sita na mwingine ana miaka minne.

SP: Nini kilikushawishi kucheza na SportPesa licha ya kuwa na kazi inayokuingizia kipato?

Yusuph: Nimeamua kucheza na SportPesa kwasababu ni njia moja wapo pia ya kuniongezea kipato ili kuweza kumudu majukumu ya kifamilia.

SP: Kitendo cha mdogo wako kupigiwa simu kuwa ameshinda bajaji na wewe ukashinda kesho yake mlikichukuliaje?

Yusuph: Yeye alishinda Jumapili na alipopigiwa simu wala hakuniambia kwasababu tunafanya kazi sehemu tofauti. Kesho yake nilipopigiwa mimi nikamwambia na ndio akaniambia na yeye kuwa amepigiwa jana ila alipatwa na mshtuko aliogopa kuniambia akidhani kuwa watakuwa ni matapeli. Kwasasa tunaamini kwasababu tumekabidhiwa na tunashukuru sana.

SP: Katika kazi yako ya ufundi huwa unaingiza kiasi gani kwa siku na unadhani bajaji hii ambayo umeshinda itakubadilishia vipi maisha?

Yusuph: Kama kazi zipo nyingi basi naweza kuingiza Sh 35,000 hadi 50,000 kwa siku na kama kazi zimeadimika basi naweza kuingiza 10,000 tu lakini nashukuru kwamba bajaji hii niliyoshinda itanisaidia kuongeza kipato cha uhakika kwa siku kwasababu biashara ya bajaji Makambako kwa sasa imeshamiri.

SP: Una neno gani kwa watanzania ambao mpaka leo bado hawaamini kwamba wanaweza kushinda bajaji?

Yusuph: Mimi nawashauri watanzania wawe na Imani kwani hivi vitu vinawezekana. Nina familia inanitegemea; wazazi, mke na watoto, na nikiwa na biashara ya bajaji itaniongezea kipato na nitaweza kumudu matunzo bila kusahau mdogo wangu ambaye pia anatarajia kupata mtoto hivi karibuni pia itamsaidia kumtunza mwanae na mkewe.

Bila shaka maisha ya ndugu hawa wawili yameshabadilika kwani kwasasa wana uhakika wa kuingiza kipato mara mbili kwa siku kama ambavyo wamesema na wataweza kutunza familia zao kikamilifu.

Kushiriki kwenye promosheni hii ya SHINDA NA SPORTPESA ili na wewe uweze kujishindia ya kwako, kwanza kabisa unatakiwa kujisajili kwa kutuma neno GAME kwenda 15888 (kama bado hujajisajili), weka pesa kwa namba ya biashara 150888 kisha piga *150*87# au tembelea www.sportpesa.co.tz kuweka utabiri wako mara nyingi.

Ukishaweka utabiri wako, utatumiwa ujumbe unaokutaka kutuma neno SHINDA kwenda 15888 ili kuingia kwenye droo. Kadri unavyozidi kucheza mara nyingi ndivyo unajiongezea nafasi ya kushinda kila siku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents