Burudani

Ndugu wanne wa muimbaji Hammer Q wafa maji ‘mwili wa baba yangu mzazi umeokotwa Tanga’

Familia ya muimbaji wa muziki wa BongoFleva na Taarab, Hammer Q imepata pigo zito kutokana na ajali ya boti iliyotokea siku tatu zilizopita na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa muimbaji huyo, amedai ajali hiyo ilitokea siku tatu zilizopita na mapema leo mwili wa baba yake mzazi umeokotwa Tanga huku wajomba zake watatu wakiendelea kutafutwa.

“Alhamdulilah mwili wa marehemu baba yangu umeokotwa pangani tanga , mda wowte utasafirishwa kwa ajili ya kuja uhifadhi katika nyumba yake ya milele 👏,” alisema Hammer Q.

Mapema leo kabla ya mwili huo mmoja kupatikana alisema “Leo ni siku ya tatu tunatafuta mwili
wa baba yetu mzazi pamoja na wajomba zangu watatu walipotea wakiwa na boti binafsi wakitokea Zanzibar kuenda Tanga,”

Alifafanua zaidi “Walikua watu 7 saba ila hapo kati walipigwa na upepo mkali na kuwatoa wote kwenye boti na boat ikaanza kuzama,”

Kwa mujibu wa maelezo ya mtu mmoja katia wawili walopatikana hai alisema “Wenzetu walitusave kwa kutupa madumu ya kuogelea ila wao hatupo nao tena na walituaga kuwa wamechoka na wameshindwa kuendelea na safari,”

Kabla ya kupatikana maiti ya baba yake Hammer Q, siku ya juzi ilipatika maiti moja na tayari imeshazikwa.

Bongo5 inatoa pole kwa familia ya Hammer Q. Innalilaah Wainnailaih Rajun

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents