Ne-Yo na mchumba wake mjamzito Crystal Renay kufunga ndoa mwezi ujao

Mwimbaji wa RnB kutoka Marekani, Ne-Yo na mchumba wake wanatarajia kufunga pingu za maisha mwezi ujao.

neyo3

Ne-Yo na mchumba wake wa muda mrefu Crystal Renay ambaye ni mjamzito hawajatangaza rasmi tarehe ya kufunga ndoa, lakini kwa mujibu wa mtu ambaye ni miongoni mwa waalikwa aliyevujisha mtandaoni kadi ya mwaliko inaonesha ndoa itafungwa February 20, 2016.

neyo ndoa-1
neyo ndoa-2

Mwezi September 2015, Ne-Yo alikanusha vuvumi ulioenea kuwa tayari walikuwa wamefunga ndoa, lakini akakiri kuwa mchumba wake ni mjamzito na kuahidi kufunga ndoa mwaka huu 2016.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW