Habari

NEC watangaza tarehe ya uchaguzi wa jimbo la Singida Mashariki lililoachwa wazi na Tundu Lissu

Image result for NEC JAJI
Jaji Semistocles Kaijage

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) leo Ijumaa Julai 05, 2019 imetangaza tarehe ya zoezi la uchaguzi wa ubunge wa jimbo la Singida Mashariki ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu ambaye alipoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa uteuzi wa wagombea utafanyika Julai 18 mwaka huu na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Julai 19 hadi 30 Julai 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa Julai 31, 2019.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti huyo amevikumbusha vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Taratibu, Miongozo, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, na Maelekezo yanayotolewa na NEC wakati wa kipindi chote cha uchaguzi huo mdogo.

SOMA ZAIDI KUHUSU TUNDU LISSU KUVULIWA UBUNGE – http://bongo5.com/hizi-ndio-sababu-kubwa-zilizopelekea-tundu-lissu-kuvuliwa-ubunge-chadema-waja-na-tamko-lau-video-06-2019/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents