Aisee DSTV!

NEC yakubaliana na maamuzi ya Mahakama, Yadai itasimamia katiba na haitawatumia Wakurugenzi wa Wilaya kusimamia uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage, amedai kuwa tume anayoiongoza haina shabiki, kada wala mwanachama hai wa chama chochote cha siasa na walikuwepo kipindi hicho imebaki kuwa historia.

Image result for jaji kaijage
Jaji Kaijage

 

Jaji Kaijage amesema hayo jana Juni 19, 2019 jijini Dar es Salaam katika semina ya wahariri na waandishi wa habari iliyoandaliwa na tume hiyo kwa lengo kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwaajili  unaotarajia kufanyika kuanzia mwezi ujao.

Kwenye tume ninayoiongoza, hakuna mwanachama hai wa chama chochote cha siasa kwa sababu NEC inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba, sheria na kanuni ziliopo,” Jaji Kaijage amesema na kuongeza “Katika tume ninayoiongoza, hakuna shabiki wala mwanachama wa chama cha siasa, kama walikuwapo ni historia siyo sasa.“.

Jaji Kaijage amesema uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa sheria na tume haiwezi kuruhusu kada wa chama kuwa sehemu ya watendaji wake na endapo wakipata taarifa za kuwapo mtu wa aina hiyo, hawatamruhusu kusimamia uchaguzi.

Pale mazingira yatalazimisha kuchukua mtu mwingine, atachukuliwa na mfano mzuri katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni, tulipata malalamiko kwa wakati kuwapo kwa mazingira ya aina hiyo, msimamizi aliyekuwa asimamie uchaguzi aliondolewa na kuteuliwa mwingine,“amesema Jaji Kaijage.

Katika semina hiyo, Jaji Kaijage amesema NEC inaheshimu uamuzi wa mahakama uliotolewa hivi karibuni kuhusu suala hilo kwa kuwa katika utekelezaji wa majukumu yake, inaongozwa na kuzingatia katiba na sheria.

Mahakama ilitimiza wajibu wake, ikavitengua baadhi ya vifungu vya sheria vilivyokuwa vimelalamikiwa, kulikuwa na vifungu maalum vilivyolalamikiwa na mahakama ikavitengua, vile vifungu vilivyolalamikiwa na vilivyotenguliwa havitatumika katika utekelezaji wa majukumu yetu,” amesema Kaijage.

Chanzo: Gazeti la Nipashe

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW