Burudani

Neema arejea nyumbani kwa masharti

Neema_msanii_face

Mama yake msanii wa filamu nchini Neema, ambaye juzi aliongea na Bongo5 kwamba mwanaye huyo ametoroka nyumbani kama wiki tatu na sisi kama chombo cha kijamii hususani katika kusaidia sanaa ya Tanzania kukua kwa kuitangaza tumeona si vibaya kumsaidia mama huyo kumrudisha mwanaye.

Mama yake Neema ametoa shukrani kwa vyombo vyote vya Habari vilivyohusika katika kutangaza baada ya kupata taarifa hii, na hatmaye mwanaye kurudi tena nyumbani. amesema  hakuna mzazi anayekubali kumdhalilisha mwanaye, lakini pia hakuna mzazi anayeweza kukubali mwanaye apotee huku akiona machoni mwake.

Mama huyo amesema kwa sasa Neema amesharudi lakini kwa mashariti kwamba, hivi sasa Neema yupo kwa mdogo wake kwaajili ya kupima vipimo vyote na baadaye kusema ni kwa nani alikuwepo ili mkumrudisha nyumbani akiwa salama na kuendelea kumtunza mwanaye ambaye bado kabisa kiumri na anastahili kuwa chini ya malezi ya wazazi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents