Burudani

Neema wa 20% amzulia balaa mama yake

Neema1
Ukiongelea kuhusu filamu ya Abas Kinzasa ’20 %’ Haki ipo Wapi? basi hutoacha kumtaja mtoto Neema, ambaye kwa kiasi kikubwa amezua msisismko kwenye filamu hiyo pale alipodondosha hisia za kweli katika sehemu ya wimbo wa ‘Ukimuona Neema,,, utamuonea huruma… hamjui baba wala hamjui mama…” hakika sehemu hiyo inavutia na kuudhunisha sana.


lakini mambo yamekuwa tofauti hivi sasa kwa mtoto huyo ambaye ndiyo kwanza anaelekea kutimiza miaka 16.  Mama Neema alinipigia simu na kuanza kulalamika huku akilia kwa madai kwamba Neema hivi sasa anamdhalilisha kwa familia kwa kitendo chake cha kutoroka nyumbani.

Mama huyo alianza kunisimulia kwa kuanza kusema, kama masihara Neema aliondoka nyumbani kama siku tatu. alijaribu kumtafuta lakini alishindwa na hatmaye akapatwa na msiba huko kwao  Arusha na kuondoka bila ya hata kumuona huku ikiwa tayari imetimia takribani wiki moja.

Anasema akiwa Arusha aliendelea kupata taarifa kwamba Neema hajarudi na wala hajatokeza nyumbani, jambo ambalo lilianza kumtia hofu zaidi. anasema kibaya zaidi hata sehemu ya mazoezi ambayo mwanaye huyo huenda kufanya mazoezi yake ya kuigiza katika kundi la Tabasam, ambalo linaongozwa na Seba na ndipo sehemu ambayo 20% alipomuona, hakuwa akitokea kabisa.

Anasema mwalimu huyo wa filamu, alimpa taarifa mama huyo kwamba mwanaye anamsimamisha mazoezi kutokana na kutoudhulia mazoezi wiki mbili mfurulizo, na hana hata dalili za kutokea kwake.

Aidha aliendelea kusimulia kwa kusema roho ilimuuma sana, kiasi cha kurudi na kujaribu kumtafuta kwa kusaidiana na kaka yake polisi wa Ostabey, lakini haikuzaa matunda. anasema siku moja mwanaye alimrushia vocha ya buku, na kumuomba kwamba amsamehe ili arudi.

Mama Neema anasema kweli roho ilimuuma sana, kwakuwa ndugu wanamuona kama vile anamfundisha tabia mbaya, hivyo alimuomba apitie kwa ndugu yoyote ili aje naye, kama vile kumuomba msamaha na ampokee ili ajirekebishe tabia hiyo.

 hapo ndipo Neema alipoongea na mke wa msanii mwenzake Niva,  na kumuomba kwamba amsindikize kwa mama yake, jambo ambalo mama Neema alilisubiri kwa hamu kwa kuwa mke huyo wa msanii alikuwa akiheshimiana naye sana.

alidai kwamba lakini Neema hakuweza kurudi wala kuonekana tofauti na alivyokuwa akisema. mama huyo anasema alipoona hivyo alijaribu kuulizia lakini wapi. Kwa sasa anasema amechoka sana na mtoto huyo kwani, amekuwa hataki kubadili tabia kwani yeye anaogopa rawama kutoka kwa baba yake  Neema ambaye anaishi Mwanza, baada ya kutengana naye.

Mama huyo anasema hivi sasa anatembea na Rb(/MAG/RB/21798/2011.06.122011), ilikuweza kumrudisha mwanaye popote alipo, kwakuwa anajua akipata mimba, maradhi kama ya Ukimwi au tatizo lolote, lazima watamfukuza na kurudi kwake na hatmaye kubeba mzigo mkubwa.

Mwisho anamalizia na kusema popote pale, na vyombo vya habari vikipata taarifa hii, viweze kumsaidia kumfikishia ujumbe kwakuwa mwanaye ni mdogo sana, na hajui anaishi na nani.

Namba ya mama Neema

0716 88 74 29

By Mo One’s

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents