Burudani

Neema yawaangukia Barack Obama na mkewe, wasaini dili nono na kampuni ya Netflix

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle Obama wamesaini dili nono na kampuni ya Netflix inayojihusisha na masuala ya burudani kwa kurusha vipindi vya TV, Series, filamu na Documentary mitandaoni.

Image result for barack obama and michelle
Barack Obama na mkewe Michelle

Obama na mkewe kwenye dili hilo wamesaini kama Mameneja wazalishaji ambapo kazi yao kubwa itakuwa ni kusimamia na kuhariri scripts za Filamu, tamthiliya na Documentary kabla ya kuruka. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NETFLIX

Hata hivyo, Obama naye baada ya kutangazwa kwa dili amesema kuwa furaha yake ni kuona anaitumikia jamii na kukutana na watu wa kila aina ili kujionea utofauti.

“One of the simple joys of our time in public service was getting to meet so many fascinating people from all walks of life, and to help them share their experiences with a wider audience. That’s why Michelle and I are so excited to partner with Netflix — we hope to cultivate and curate the talented, inspiring, creative voices who are able to promote greater empathy and understanding between peoples, and help them share their stories with the entire world.”

Licha ya Netflix kutangaza dili hilo mpaka sasa hawajaweka wazi ni kiasi gani watawalipa wawili hao, kampuni hiyo imekuwa ikiwalipa watu maarufu mamilioni ya dola kwenye mikataba yake.

Kampuni ya Netflix mwaka 2014 ilitangaza rasmi kuingia barani Afrika lakini hata hivyo haijapata umaarufu zaidi ukilinganisha na mabara mengine.

_______________________________________________________________________________________________

Kwa sasa unaweza kupata habari zetu zote sehemu moja kwa kupitia App yetu ya Bongo5. Pakua sasa kupitia Play Store kwa kubonyeza link hii – https://bit.ly/2J2Argw

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents