Nelson Mandela alazwa tena

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa kwenye hospitali ambayo bado haijajulikana bado. Alilazwa jana usiku kutoka na maambukizi sugu ya mapafu.

mandela

Msemaji wa serikali Mac Maharaj amesema kwenye maelezo yake kuwa madaktari wanamhudumia vizuri na kwamba anapata matibabu yote yanayowezekana. Rais Jacob Zuma amemtumia salamu za ugua pole.

“Tunawaomba wananchi wa Afrika Kusini na duniani kote kumwombea mpendwa wetu Madiba na familia yake na kuwakumbuka kwenye fikira zao,” alisema Zuma kwenye maelezo yake.

Maharaj ameomba watu wawe na uelewa na kuwapa nafasi madaktari wafanye kazi yao. Mandela ana historia ya matatizo ya mapafu baada ya kuugua kifua kikuu mwishoni mwa miaka 27 aliyokuwa jela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents