Burudani

Nene Leakes kurudi tena kwenye “RHOA”

Kama wewe ni mfuatiliaji wa ‘reality TV’, basi jina la Nene sio geni kwako, na kama hufatili ni kwamba mwana mama huyO asieisha vituko na ukorofi, ataoneka kwenye kipindi cha “The Real Housewives of Atlanta” (RHOA).

Nene Leakes anatarajiwa kuonekana upya kwenye msimu wa kumi wa kipindi cha ‘The Real Housewives of Atlanta” , kipindi hicho kinachoonyesha maisha ya wanawake tajiri wa mji wa Altlanta wanavyoishi kila siku.

Mmoja wa watu anaehusika katika utengenezaji wa kipindi hicho ameueleza mtandao wa TMZ kuwa,Nene yupo tayari kurudi kwenye show hiyo lakini bado hajasaini mkataba rasmi

“Kuna utata wa pesa, Nene anataka kulipwa zaidi ya wenzake wakiwemo Kim Zolciak .Tunategemea kumrudisha kama moja wa washiriki wa muda mfupi kwenye RHOA kwa mara nyingi kama ilivyo kwa Kim” alisema mtu huyo.

Na Laila Sued.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents