Habari

New Couple Alert: Hussein Machozi na Size 8 wa Kenya ‘Tunapendana ki Uhakika’


Sababu iliyopelekea msanii wa Bongo Flava Hussein Machozi kupageuza jijini Nairobi, Kenya kama uwanja wa nyumbani hatimaye imejulikana.
Hussein ameiambia Bongo5 ‘exclusively’ kuwa he has found his love in Kenya. Na msichana mwenye bahati ya kuitwa shemeji/wifi na watanzania si mwingine bali ni mwanamuziki maarufu nchini humo Linet Masiro Munyali aka Size 8. Hapo ndipo tunaweza kupata majibu ya kwanini hivi karibuni alisema anafikiria kuhamia moja kwa moja nchini Kenya.Imetokea tu kama bahati mbaya ama nzuri mwandishi wa habari hii ni mtu wa karibu mno na Hussein na hivi ndivyo maongezi yalivyokuwa:
Hussein: Asee eti naskia wabongo wanadai nimeolewa na size 8..umezipata hizo?
Mwandishi Bongo5: Sijapata mwanangu, kwani unamla huyo mtoto?
Hussein: haha! wacha nikwambie ukweli man, kitambo sana tumeanza kuwa pamoja ila sa sijui nani kazitoa hizo!
M/Bongo5: Dah kumbe! Hongera sana mwanangu, so mnakaa pamoja?
Hussein: hahaha! mara nyingi huwa tupo pamoja japo kila mtu anakaa kwake.
M/Bongo5: Kwani hutaki watu wajue?
Hussein: aah! wanaeza jua ila sio ka wanavyo sema eti nimeolewa asee!
M/Bongo5: Mlikutana wapi na Size 8? Katika mazingira gani yaani?
Hussein: Kawaida, kuanza kuchat na tukawa marafiki hatimaye imekuwa hivyo.

M/Bongo5: Ndio sababu hutaki kuhama Kenya nini?
Hussein: haha! kama unavyojua hakuna mtu anayetaka kukaa mbali na pumzi yake yeye ni sababu kubwa ya mimi kuwa Kenya.
M/Bongo5: Lini unampeleka Singida kwa mama?
Hussein: Coz mi nimekuja kwao naye soon ataenda SINGIDA, MANYONI kujitambulisha.
M/Bongo5: Mna mipango ya kuja kuwa mtu na mke wake kabisa?
Hussein: Yes mipango ni kuwa mke na mume maana hakuna anayetaka kucheza na roho ya mwenzake..
M/Bongo5: So,unazizungumziaje tetesi kuwa Size 8 amekuoa na ndo anakuweka mjini Nairobi?
Hussein: haha! ni uvumi tu mwana kwani mi kukaa kwa mpenzi wangu ndo kusema amenioa? Okay, sasa atakuja TZ KWANGU tusikie watasemaje. Mwisho nasisitiza man tunapendana ki uhakika.
There you have it! Congrats Hussein, nice choice!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents