Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

New Music: Chin Bees – Pepeta

Rapper Chin Bees, ameachia video ya wimbo wake mpya Pepeta, ikiwa ni mradi wa kwanza chini ya label ya muziki nchini, Wanene Entertainment. Pepeta, wimbo wa kwanza kutoka kwenye album yake itakayotoka mwaka huu, ni trap inayotabiriwa kuja kuwa ‘anthem’ si tu redioni, bali mtaani na zaidi kwenye klabu na viota vya burudani.

Pepeta ni wimbo unaobeba maana halisi ya muziki wa kileo wa vijana wa mjini na wenye lengo moja tu, kufurahi na kula bata huku ukisahau shida zote. Wimbo huo umetayarishwa na producer wa Marekani, Thomas Crager huku mastering ikifanyika katika studio za Wanene chini ya mikono ya mjuzi wa fani hiyo, Sarthak (sound engineer).

“Video ya Pepeta imefanyika chini ya director Rahul, lights na shots zile amefanya mtu mmoja anaitwa Aanand Lonkar,” anasema Chin Bees. Chin anayejulikana kwa uwezo wake wa kufanya karibu aina zote za muziki, anasema Pepeta ameipa mahadhi ya trap ili kuendelea kuonesha namna
anavyobadilika kama kinyonga hasa baada ya nyimbo zake zilizopita ukiwemo Zuzu, kuwa na mahadhi ya Zuku.

“Nataka kuwa mtu wa kutofanya style moja, mimi nataka niwe nafanya style tofauti na kila moja niifanye kwa ubora mzuri,” anasema Chin. “Pepeta sio trap ambazo tunazisikia kwenye game, ni trap tofauti, kuanzia video, mastering ya audio, zote ziko perfect.”

Chin Bees anasema ukubwa wa mradi wake wa Pepeta usingefanikiwa bila nguvu kubwa iliyowekwa na uongozi wake wa Wanene. “Namshukuru Mungu, pia uongozi wangu kwa kitu kama hicho.” Pamoja na Pepeta kuja na video yenye kiwango cha kishindo, Chin Bees anatambulisha pia uchezaji mahsusi kwaajili yake ambao kwa vijana wenye uwezo wa kucheza watapata fursa ya kushiriki kwenye #PepetaDanceChallenge na kujishindia zawadi kibao.

Kwa wakazi wa Dar es Salaam watapata fursa ya kuona mabango ya video barabarani katika takriban maeneo saba yanayoonesha ratiba mbalimbali za mahojiano ya redio na TV na Chin Bees na kuifanya kuwa aina ya promotion ya kipekee katika tasnia ya burudani nchini Tanzania.

KUHUSU CHIN BEES

Chin Bees ni rapper na muimbaji mwenye vipaji vingi hususan utunzi na uandishi wa nyimbo, na uwezo wake wa kufanya muziki wa aina nyingi. Amejipatia umaarufu si kwa nyimbo zake pekee, bali pia kwa kuimba viitikio kwenye nyimbo zilizofanya vizuri zikiwemo Sweety Mangi na Role Model za Nick wa Pili na Arosto ya G-Nako. Amewahi pia kushiriki kuandika nyimbo za wasanii wakubwa wakiwemo Vanessa Mdee na Navy Kenzo. Nyimbo zake zilizowahi kutamba ni pamoja na Pakaza aliyomshirikisha G-Nako, Simanzi aliyomshirikisha Ben Pol, Let Me Know aliyowashirisha Navy Kenzo, Zuzu na Ruba.

KUHUSU WANENE ENTERTAINMENT

Wanene Entertainment Ltd ni kampuni iliyojikita katika utengenezaji wa maudhui na inayotumia vifaa vya kisasa ili kuzipa uhai kazi za muziki, video na graphics kupitia timu yake yenye wajuzi wa fani hizo. Kwa kutumia uzoefu katika burudani ya sauti na video, Wanene inafanya kazi kwa kufikia vigezo vya tasnia vinavyokubalika kimataifa. Wanene ni studio kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati, inayoipa fursa kanda hii utayarishaji wa kutukuka kwa gharama nafuu. Wanene imepanga kuendelea kuvumbua mbinu katika sauti na video ili kwendana na changamoto kwenye sekta ya burudani kuhakikisha kuwa wateja wanapata kazi zenye ubora kwa malipo nafuu.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW