DStv Inogilee!

New Video: Jay Fernando – My Life

Tazama video ya ngoma mpya ya rapper wa Burundi anayeishi nchini Ubelgiji, Jay Fernando – My Life.

Chini ni Historia yake fupi:

Nahimana Junior, maarufu kama Jay Fernando alizaliwa tarehe 27/09/1989 katika tarafa ya Buyenzi mjini Bujumbura nchini Burundi. Aliishi maisha ya kawaida kama watoto wengine wa maisha ya chini katika kushiriki michezo, shule na kadhalika. Alianza kujishirikisha na masuala ya muziki mnamo mwaka 2003 baada ya kuvutiwa kwa muda mrefu na tasnia hiyo iliyokuwa kwenye familia yake.

Atakumbukwa marehemu binamu yake W.Dog ambaye alikua muimbaji maarufu na muanzilishi wa kundi la nyimbo za kufoka “Rap” lilofahamika kama “Nigga Soul Familly na alitia fora sana mnamo miaka ya 1998 hadi 2000 na kusambaratika baada ya kifo chake.

Jay Fernando tayari amekwishashiriki kwenye nyimbo saba huku akiwa na nyimbo zake binafsi tatu. Nyimbo hii ya “My life” ndio ya kwanza aliyoitoa pekee yake. Nia yake ni kutaka kuutambulisha muziki wa Burundi kimataifa. Jay Fernando kwa sasa anaishi nchini Ubelgiji na tayari ni baba wa mtoto mmoja wa kiume.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW