Videos

New Video: Lil Wayne – God Bless Amerika (Very Hot)

Watakuja Rappers wapya watahit, watashine, watapendwa na watakamata chart duniani lakini bado Lil Wayne ataendelea kuwa ‘rapper bora aliyehai katika muda wake’. Lil Wayne amekuja tena kwa kishindo kuchafua amani kwa video hii kali ya wimbo wake ‘God Bless Amerika’ uliopo kwenye albam yake, I Am Not a Human Being II.

http://www.youtube.com/watch?v=mrt66B8GOr0

Video hii ameishoot New Orleans ambako ndiko anatokea. Weezy anaonesha sura halisi za wananchi wa mji huo wanavyoishi maisha magumu baada ya kuharibiwa vibaya na kimbunga cha Katrina kilichopiga eneo hilo kuanzia August 23, 2005 – August 30, 2005. Kwenye video hii wanaonekana pia Birdman na Mack Maine.

Kama unakumbuka wakati akishoot video hii iliyoongozwa na Eif Rivera, Lil Wayne alizua mzozo baada ya kuonekana akiikanyaga bendera ya Marekani japo kwenye video hii hakuna sehemu inayoonekana akifanya hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents