DStv Inogilee!

New Video: Navy Kenzo waachia video mpya ‘Kamatia’ iliyofanywa na Campos Afrika Kusini

Kundi la muziki la Navy Kenzo linaloundwa na producer Nahreel na Aika ambaye pia ni girlfriend wake, wamewapakulia chakula kingine mashabiki wao kwa kuachia single mpya iitwayo ‘Kamatia’ usiku wa kuamkia January 30, 2016.

Navy Kenzo - kamatia cover

Video hiyo imetayarishwa na director aliyeongoza video yao iliyopita, ‘Game’ – Justin Campos wa kampuni ya Gorilla Films ya Afrika Kusini.

Kwa mara nyingine ukiusikiliza wimbo huu utagundua kuwa Navy Kenzo wameamua kuendeleza mahadhi ya wimbo wao uliopita ‘Game’, baada ya kushuhudia ukipata mapokezi mazuri na kushika chati mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania.

Kabla ya kuiweka mtandaoni video ya ‘Kamatia’ , Aika na Nahreel waliitambulisha video hiyo kwa kushitukiza usiku wa kuamkia leo (January 30, 2016) walipohudhuria kwenye party ya ‘No Tie After Five’.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW