Burudani ya Michezo Live

New Video: Stereo Heroes (Kenya) – Tuko Juu

Kwa ubunifu udhihirishao ustadi mkubwa wa kisanii, wamejumuisha mitindo kem kem ya kimuziki, mingine ya kiafrika na mengine ya ughaibuni katika nyimbo zao na iwapo hujapata habari, Stereo Heroes, wasanii watokeao Nairobi, Kenya wamekuja tena kwa kishindo kikubwa.

Wamekuwepo kwa muda sasa na inavyoonekana, wanamuziki hawa wanaupa muziki wa Nairobi dira mpya. Inajulikana wazi kwamba uanamuziki ni fani yenye ushindani usio kifani na wasanii hufanya kila hila kufanikisha juhudi zao za kung’aa.

Sikiliza na tazama video yao mpya ya wimbo Tuko Juu ushuhudie ujio wa vijana hawa ulingoni.

Tunahisi hii ndio ‘hit’ mpya ambayo haitafunika Nairobi tu, bali hata kanda nzima ya Afrika ya Mashariki na kati. Heko Stereo Heroes.

Unaweza kuwafollow Twitter na Instagram kwa jina @StereoHeroesKe na Facebook hapa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW