Habari

New Zealand: Watu watano wamepoteza maisha na wengine 31 kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa volkano – Video

New Zealand: Watu watano wamepoteza maisha na wengine 31 kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa volkano - Video

Polisi nchini New Zealand imesema hakuna dalili ya kuwapata manusura baada ya mlipuko wa volkano kutokea siku ya Jumatatu. Mlipuko wa volkano nchini New Zealand, umesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine kadhaa hawajulikani walipo, polisi inasema.

Watalii walionekana wakitembea karibu na mlima huo muda mfupi kabla ya mlipuko kutokea.

Polisi inasema watu 23 wameokolewa, lakini imetahadharisha kuwa idadi ya waliofariki ”huenda” ikaongezeka.

Eneo hilo kwa sasa ni hatari kuendesha shughuli zozote za uokoaji.

Kisiwa cha White Island, ambacho pia kinafahamika kama Whakaari, ni moja ya maeneo yalio na milima mingi ya volkano.

Licha ya hivyo, kisiwa hicho huwavutia watalii ambao huzuru mara kwa mara nyakati za mchana kutokana na kuwepo kwa ndege zinazoendesha shughuli za kitalii.

Nini kilichotokea katika volkano?

Mlipuko wa volkano katika eneo la White Island ulianza saa 14:11 sa za New Zealand (01:11 GMT).

Mgeni Michael Schade – ambaye alikuwa akitumia boti kuzuru kisiwa hicho nyakati za asubuhi alinasa video ya jivu na moshi mzito baada ya volkano kulipuka.

Presentational white space

Aliiambia BBC kwamba alikuwa karibu na mlima huo dakika 30 kabla ulipuke.

“Ilikuwa bado ni salama kwa kiwango fulani lakini wasimamizi walikua wakidhibiti idadi ya watu wanaozuru eneo hilo lenye mlima wa volkano.”

Akielezea mlipuko huo, alisema: “tulikuwa ndio mwanzo tumeingia ndani ya boti…na punde tu baada ya hapo mtu akatugusia tulichokiona. Tshutuka sana kusema kweli.

“Tuligeuza boti na kuwachukua watu waliokuwa wakisubiri kuabiri na kurudi tulikotoka.”

Shuhuda mwingine, Mbrazili Allessandro Kauffmann, aliponea chupu chupu kuungua kutokana na moto wa majabali yalioyeyuka kutoka katika mlima huo.

Picha za moja kwa moja kutok aeneo la tukio muda mfupi baada ya mlima volkeno kulipika
Image captionPicha za moja kwa moja kutok aeneo la tukio muda mfupi baada ya mlima volkeno kulipika

Nani aliyefika katika kisiwa hicho?

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amesema kulikuwa na ”watu kadhaa” miongoni mwao watalii ambao walikuwa wanazuru eneo hilo, kutoka New Zealand na ughaibuni.

“Najua jamaa za watu waliokuwa katika kisiwa hicho watakuwa wamejawa na hofu na wasiwasi kuhusu usalama wao – lakini nawahakikishia kuwa polisi inafanya kila iwezekanalo kuwasaidia,” alisema.

Aliongeza kuwa polisi imeanzisha oparesheni ya kuwatafuta manusura lakini moshi mkali katika eneo hilo unakatiza juhudi hizo.

Map of White Island

Mlipuko huo ulitarajiwa?

Tarehe tatu mwezi huu wa Disema, wataalamu wa jiolojia wanaochunguza wavuti wa GeoNet walionya kuwa “tmlima huo wa volkeno huenda ukalipuka kupita ilivyo kawaida yake ,” japo waliongeza kuwa “viwango cha sasa cha milipuko hiyo hakiwezi kuhatarisha maish aya wageni wanaozuru mlima huo”.

Kisiwa cha White Island kimeshuhudia milipuko kadaaa ya volkeno katika miaka iliyopita, ya hivi karibuni ikiwa na mwaka 2016, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Polisi inaonya watu wanaoishi karibu na na maeno ya hayo kuwa ”waangalifu dhidi ya majivu ya moto na kuwaomba ikiwezekana wasiondoke majumbani mwao”

Mlipuko huu wa sasa hautarajiwi kuathiri kiswa cha kaskazini, huku majivu na mabaki ya miamba iliyoyeyuka ikitarajiwa kufika nchi kavu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents