Michezo

Newcastle ya kamilisha usajili wa Andros Townsend kutoka Tottenham Hotspur

Klabu ya Newcastle United imefanikiwa kumsajili winga wa kimataifa wa Uingereza Andros Townsend kwa gharama ya pauni milioni 12 akitokea Tottenham Hotspur.

30A3BFA800000578-3419531-image-a-32_1453920105760

Winga huyu mwenye miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano kukitumikia kikosi cha Newcastle chini ya meneja Steve Mclaren.

30A3BDE100000578-3419531-image-a-30_1453920011250

Townsend katika msimu huu amecheza michezo mitatu akitokea benchi huku akiondolewa katika kikosi kilichokua kinashiriki michuano ya Europa ligi baada ya kugombana na kocha wa viungo Nathan Gardiner.

Meneja wa Newcastle United Steve McClaren, Amesema”kumleta winga huyu katika timu hiyo ni usajili mzuri na mkubwa, Andros ni aina ya mawinga wanaocheza staili ya kizamani anaweza cheza kulia na kushoto .”

Townsend alijiunga na kituo cha michezo cha Spurs akiwa na miaka nane na alianza kukitumiki kikosi cha kwanza katika msimu wa 2013-14

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents