Neymar ajitetea baada ya kuonekana kituko ‘Nilikuwa najiskia maumivu makali mno’

Mshambuliaji wa Brazil, Neymar amejitokeza na kujetetea juu ya kitendo chake cha kuonekana kama amejigaragaza mno wakati alipochezewa faulo na Miguel Layun ukilinganisha na namna hata tukio hilo lilivtokea, hayo yamekuja baada ya kupata lawama nyingi kutoka kwa wapenzi wa soka na baadhi ya mitandao ya kijamii.

Neymar mwenye umri wa miaka 26 amejitupatupa mno alipochezewa faulo na mchezaji wa timu ya taifa ya Mexico, Miguel Layun mchezo wa 16 bora wa kuwania kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia na kumalizika kwa matokeo ya Brizil kupata shindi wa mabao 2 – 0.

Mchezaji huyo ghali zaidi duniani anayekipiga kwenye klabu ya Paris St-Germain amesema kuwa alikuwa akijiskia maumivu makali.

“Nilikuwa najiskia maumivu makali mno, nilikuwa nashindwa hata kujizua kwa vile nilivyokuwa najiskia,” amesema Neymar.

Kocha wa tim ya taifa ya Mexico, Juan Carlos Osorio kwa upande wake amesema kuwa mshambuliaji huyo aliigiza mno na siyo mfano mzuri wa kuigwa kwenye soka.

Carlos Osorio ameongeza kwa kusema ni haibu katika mchezo wa soka, watu wamepoteza muda mwingi kwa sababu ya mchezaji yeye mmoja tu.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW