AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Neymar asahau majeraha, abwaga magongo chini na kuanza kurukaruka kwa furaha PSG ikiiadhibu vikali Man United (+video)

Mchezaji ghali zaidi duniani, Neymar amejikuta akisahau majeraha ya mguu nakuanza kuruka ruka kwa furaha wakati klabu yake ya Paris Saint – Germain ikiifunga Manchester United mabao 2 – 0 kwenye mchezo wa UEFA Champions League uliyopigwa usiku wa Jumanne.

Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil hakujali majeraha aliyokuwanayo na badala yake alianza kurukaruka kwa furaha na hata kuukanyagia mguu wake wenye majeraha baada ya timu yake ya PSG ikiifunga United kwenye dimba la Old Trafford. 

Kipande cha video ambacho kipo kwenye mtandao wa OTRO kinamuonyesha staa huyo mwenye umri wa miaka 27, akiruka ruka kwa furaha baada ya kuingia kwa mabao hayo mawili.

Presnel Kimpembe alianza kupachika bao la kwanza dakika ya 53 kisha Kylian Mbappe akamalizia karamu ya magoli baada ya kutupia dakika ya 60 ya mchezo wakati huo, Neymar akishuhudia kupitia luninga.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW