DStv Inogilee!

Neymar ashindwa kujizuia, atokwa na machozi akimzungumzia Lionel Messi ‘Kila ninapohitaji msaada hujitokeza na kunishika mkono’

Mchezaji ghali zaidi duniani, Neymar ameeleza kwa hisia kubwa namna alivyokuwa akipata msaada kutoka kwa nyota wa Barcelona, Lionel Messi wakati alipokuwa akiitumikia timu hiyo.

Kwenye mahojiano yaliyofanya na Rede Globo’s Esporte Espetacular (via Diario AS), nyota huyo wa Paris Saint-Germain, Neymar mwenye umri wa miaka 27 ameonekana akibubujikwa na machozi kwakuzungumzia ubinadamu na ukarimu aliyokuwa akiupata kutoka kwa Messi kipindi cha maisha yake ya Barcelona.

”Ni stori ninayomuambia kila mtu, wakati huo ninapohitaji sapoti Barca, mtu anayejitokeza kunisaidia kwenye timu, basi ni mchezaji bora kabisa duniani, hujitokeza na kunionyesha upendo, mara zote hujitokeza na kunishika mkono na kusema nipo hapa kwaajili ya kukusaidia.” Meymar amezungumza hayo kwenye mahojiano yake na Globo Esporte.

”Huzungumza na mimi na kuniambia, njoo hapa, nilazima uwe wewe, ni lazima uwe na furaha, usinihofie au mtu yoyote ndani ya hii klabu tupo hapa kwaajili kukusaidia wewe.”

Mbrazil huyo bado anahusishwa na kurejea Nou Camp kujiunga tena na marafiki zake wa Barcelona.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW