Michezo

Neymar atupia goli la mwaka akiiongoza PSG dhidi ya Guingamp (Video)

Mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa raia wa Brazili, Neymar amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika mchezo wake wa kwanza akiwa anaitumikia klabu yake mpya ya Paris St-Germain baada ya kununuliwa kwa rekodi ya dunia ya paundi milioni 200 akitokea Barcelona.


Neymar alichangia katika mabao yote matatu ambayo yamefungwa na timu yake ya PSG ilipocheza dhidi ya Guingamp ambapo wamefanikiwa kudumisha rekodi yao ya kushinda 100% mwanzo wa msimu.

Mchezaji wa timu ya Guingamp, Jordan Ikoko ndiye aliefungua ukurasa wa mabao kwa kujifunga baada ya pasi ya Neymar kwa Edinson Cavani kuzimwa.

Mchezajio huyo hghali zaidi, Neymar kisha alimsaidia Cavani kufunga kwa pasi safi kabla ya nyota huyo wa uruguay naye kumpa pasi Neymar ambaye alifunga dakika za mwishomwisho akiwa hatua sita hivi kutoka kwenye lango.

Neymar mwenye umri wa miaka 25, alichezeshwa upande wa kushoto lakini alihusika katika safu ya mashambulizi.

Alicheza katika kiwango cha hali ya juu huku akipiga mashuti langoni mwa timu pinzani, ingawa mengi ya makombora yake yalizimwa kabla yake kufanikiwa kufunga katika dakika za lala salama.

Hizi ndizo takwimu za Neymar katika mchezo wake wa kwanza akilinganishwa na washambuliaji wa timu hiyo
Edinson Cavani na Angel di Maria

Mashuti sita, pamoja na yaliyozimwa(sawa na Cavani na Di Maria)
Neymar katika mchezo huo amefanikiwa kupiga pasi 88
Wakati, Cavani amepiga pasi 21, huku Di Maria akipiga pasi 63.
Neymar amepiga pasi kwa ufasaha kwa 76%
Wakati, Cavani aamepiga pasi kwa ufasaha 91%, na Di Maria 86%
Pasi muhimu7 (Cavani 2, Di Maria 0)
Kukabili wapinzani22 (Cavani 4, Di Maria 7)
Kufanikiwa kukabili wapinzani 73% (Cavani 50%, Di Maria 29%)
Kupoteza mpira 33 Cavani 6, Di Maria 13

https://www.youtube.com/watch?v=W9fMnfXoz5c

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents