Michezo

Neymar aweka wazi mchezaji anayemkubali kati ya Ronaldo na Messi ‘Yeye ni role model wangu’

Nyota wa klabu ya Paris Saint-Germain, Neymar amemwagia sifa mshambuliaji bora duniani na mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Lionel Messi kuwa ndiye mchezaji bora wa muda wote kwa upande wake.

Neymar ameyasema hayo wakati alipokuwa na nyota wa NBA, Stephen Curry wakati alipoulizwa kuhusiana na maisha yake katika soka pamoja na wachezaji wenzake maarufu, Ronaldo na Messi.

(kushoto) Neymar, Messi na Ronaldo

”Nimekutana na Messi na Cristiano Ronaldo, nimewahi kucheza na Messi ambaye kwangu mimi ndiyemchezaji bora wa muda wote na kwa upande wangu ndiyo ‘role model’ wangu kwenye soka,” amesema Neymar.

”Kwa Messi ninajifunza kila siku eidha kwenye mazoezi, wakati ninapochezanaye au ninapomtazama akiwa anacheza uwanjani. Hivyo hunifanya niwe imara na kuongeza uwezo wangu ndani ya uwanja kwasababu najifunza vitu vingi kutoka kwake.”

”Kwa Cristiano Ronaldo huyu jamaa ni hatari kukutana naye uwanjani na niheshima lakini ni lazima tuwe tumejiandaa vya kutosha. Ni mmoja kati ya wachezaji bora kabisa duniani hivyo ukikutana naye lazima uwe makini na tahadhari kubwa lakini pia wakati huo huo unajifunza kutoka kwake pia.”

”Kwa hiyo ni miongoni mwa wachezaji wawili wakubwa ambao naweza kuwalinganisha kwasababu nahitaji kujifunza zaid kutoka kwao, nahitaji zaidi mataji, kufunga zaidi kwahiyo naendelea kujifunza kila siku.”

Neymar amesajiliwa na matajiri wa Ufaransa klabu Paris Saint-Germain kwa dau la euro milioni 222 ambayo ni sawa dola za Kimarekani milioni 263 akitokea Barcelona.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents