Neymar azua gumzo mtandaoni baada ya kushangilia hivi (+Picha)

Neymar amekuwa akiangazwa zaidi toka alipojiunga na matajiri wa Ufaransa klabu ya PSG kwa dau nono la paundi milioni 200 na kwa sasa amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuonyesha staili yake mpya ushangiliaji.

Baada ya kushinda bao lake hilo kwanjia ya mkwaju wa penati akaweka kiatu chake chenye chata la Nike katika paji la uso wake kitendo ambacho kimetawala katika vichwa vya habari huku watu wengi wakitumiana picha hiyo.

Katika mchezo huo Neymar, Kylian Mbappe na Angel Di Maria wote wametupia mara mbili na kuifanya Paris Saint-Germain kutoka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Rennes katika michuano ya French Cup siku ya Jumapili.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW