AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Neymar Jr atuma maombi ya kurudi Barcelona, Coutinho abaki tumbo joto

Mshambuliaji wa klabu ya PSG ya Ufaransa, Neymar Jr ametuma maombi ya kurejea FC Barcelona, ikiwa ni misimu miwili imepita tangu aihame klabu hiyo.

Related image
Neymar Jr

Kwa mujibu wa gazeti la EL Mundo Deportivo la Hispania, limeeleza kuwa baba yake na Neymar ameshatuma maombi ya mtoto wake kurudi kwenye klabu hiyo.

Gazeti hilo limeeleza kuwa, Barcelona wamekubali ombi lake, lakini kwa masharti ya kumtaka afute kesi ya madai ya Euro Milioni 30, ambayo anaidai klabu hiyo tangu alivyovunja mkataba wake mwaka 2017.

Imeelezwa kuwa Neymar Jr kwa sasa hana furaha na timu yake ya PSG.

Wakati hayo yakijiri, mshambuliaji wa mabingwa hao wa Hispania, Phillipe Coutinho yupo mbioni kuuzwa na klabu hiyo ili kupunguza gharama za usajili wa Neymar.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW