Michezo

Neymar sasa kutambulishwa rasmi leo – PSG

Matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Brazil, Neymar kwa ada iliyoweka rekodi mpya ya Euro milioni 222 sawa na pauni milioni 200 kutoka Barcelona.

Ununuzi huo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 umevunja rekodi ya awali iliyowekwa na Paul Pogba aliporejea Manchester United kutoka Juventus kwa pauni milioni 89 mwezi Agosti 2016.

Neymar atakuwa analipwa Euro milioni 45 sawa na pauni milioni 40.7 kwa mwaka nakulipwa  Euro 865,000 sawa na pauni 782,000 kila wiki hii ikiwa ni kabla ya kutozwa ushuru katika mkataba wake wa kwanza wa miaka mitano. Hiyo ni jumla ya pauni milioni 400.

Neymar amesema amejiunga na “mojawapo ya klabu zenye ndoto kuu zaidi Ulaya”.

“Ndoto kuu ya Paris St-Germain ilinivutia kujiunga na klabu hiyo, pamoja na kujitolea kwao na nguvu zinazotokana na hili”. Najihisi niko tayari kuanza kazi. Kuanzia leo, nitafanya kila niwezalo kuwasaidia wachezaji wenzangu wapya.” Amesema Neymar.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Ufaransa imepanga kuwa na kikao na wanahabari leo siku ya Ijumaa saa nane unusu kwa saa Afrika Mashariki.

Neymar  atatambulishwa rasmi kwa mashabiki wa PSG Jumamosi wakati wa mechi yao ya kwanza kabisa ya msimu mpya, ambapo watakuwa katika uwanja wa nyumbani wa Parc des Princes wakicheza dhidi ya Amiens.

 

Kifungu kilichokuwa kinazuia kumwachilia mchezaji huyo katika mkataba wake kinaweza kufunguliwa kwa Neymar kulipa pesa yeye binafsi.

Wakati alipofika na pesa nchini Hispania hapo jana kwaajili ya kulipa maafisa wa La Liga walikataa malipo hayo.

Hali iliyosababisha kutokea kwa majibizano kati ya maafisa wa La Liga na wasimamizi wa Ligue 1.

La Liga wanaamini PSG huenda wanakiuka sheria za uchezaji (FFP) kwa kumnunua mchezaji huyo wa Brazil.

Baada ya kushindwa kulipa pesa hizo kwa La Liga, wawakilishi wa Neymar walilipa Euro milioni 222 sawa na pauni milioni 200 katika ofisi za Barca.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Brazili alijiunga na Barca mwaka 2013 na kuisadia timu hiyo kushinda mataji mawili ya La Liga na moja la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Matajiri hao wa Ufaransa PSG wanashika nafasi ya 11 kwa klabu zenyethamani duniani kwamujibu wa Forbes lakini ni mara yao ya kwanza kuvunja rekodi ya dunia kwa usajili wa Neymar.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents