Michezo

Neymar sasa ni Neymoney, paundi milioni 357 kumpeleka Madrid

Aliyekuwa mchezaji wa Barcelona anayekipiga kwa matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain inayomilikiwa na mfanyabiashara kutoka Falme za kiarabu, Sheikh Nasser bin Ghanim Al-Khelaïfi, Neymar Jr huwenda akatimkia Santiago Bernabeu na kufanikiwa kuvunja rekodi aliyoiweka ya usajili wa paundi milioni 200 wakati alipotua katika timu hiyo.

Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez huwenda akamsajili mshambuliaji huyo wakimataifa wa Brazili baada ya kumzungumzia mwezi mmoja tu tangu Cristiano Ronaldo ajinyakulie taji lake la tano la Ballon d’Or.

Fowadi huyo wa PSG, Neymar tayari amefanya mazungumzo na wakala wake na kumuomba kutimiza dili hilo la kuhamia Real Madrid.

Ripoti zinasema kuwa kilakitu kinakwenda sawa ila Madrid italazimika kutoa dau la paundi milioni 357 ikiwa ni pamoja na ada ya uhamisho kama watahitaji kuishawishi PSG kumuachia.

Rais huyo wa Madrid, Florentino Perez amesema kuwa  “Kuwa ndani ya Madrid hukuwezesha kushinda taji la Ballon d’Or kirahisi. Madrid ni timu inayowawezesha wachezaji wakubwa kupata kilakitu wanachokihitaji, kila mtu anafahamu hilo nahitaji kumsajili,” Perez amesema wakati akizungumzia lengo la Neymar hasa kunyakuwa taji hilo.

Kwamujibu wa habari kutoka gazeti la Marca la nchini Hispania mchezaji huyo ghali zaidi dunia kwa sasa gharama yake ya kuhamia Madrid itakuwa paundi milioni 357 na hii inakuja baada ya kuchukua takribani miezi sita tu tangu Mbrazili huyo kutua PSG.

Kwamara ya kwanza Neymar aliwahi kufanya mazoezi na Madrid akiwa na umri wa miaka 14 wakati nyota wa timu hiyo kwa wakati huo akiwa Dani Carvajal.

Ingawa mchezaji huyo alifanya maamuzi ya kurejea kwao Brazili. Mwaka 2013, Real Madrid kwamara nyingine tena walimuita Neymar nakufanikiwa kufaulu vipo vya afya lakini aliamua kutimkia Barcelona. Sasa ni mara ya tatu Real Madrid wanajaribu bahati yao ya kumsajili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents