Uncategorized

Ngassa amjibu aliyekuwa msemaji wa Yanga, Jerry Muro ‘Kwetu tumefundishwa mkubwa hakosei’

Mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na aliyewahi kuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kuonyesha kutofurahishwa na matokeo waliyopata mabingwa hao wa kihistoria ya kufungwa bao 1 – 0 na mtani wake Simba hali iliyopelekea hadi kusema kuwa mchezaji Moshi ‘Boban’ na Mrisho Ngassa si wachezaji wanaopaswa kuitumikia timu hiyo.

Hatimaye mchezaji wa klabu hiyo Mrisho Ngassa amezungumzia kali hizo zilizotolewa na Mh Jerry Muro kupitia mahojiano yae na Radio EFM ”Kwanza naanza kumshukuru Mwenyezi Munngu kwa matokeo, na kikosi siyo kwamba kibaya ni kizuri. Nilipofika nyumbani watoto wangu waliniambia baba tunakuja kukuangalia na tunaimani unaweza kushinda katika mechi ya leo,” maneno ya Mrisho Ngassa baada ya kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Mbao FC hapo jana.

Alipoulizwa anaizungumziaje kauli ya iliyotolewa na aliyewahi kuwa Msemaji wa Yanga, Jerry Muro juu ya uwepo wake ndani ya kikosi cha Yanga, Ngassa amesema ”Kwetu tumefundishwa mkubwa hakosei, hivyo mimi siwezi kumlaumu kwasababu kipaji chake ni kuongea na mimi kipaji changu ni kucheza mpira.”

”Na pia katika mpira kuna kutukanwa kwahiyo ukiwa staa lazima ujue kuangalia mabaya, staa siku zote anatukanwa, anasimangwa lakini kikubwa namshukuru Mwenyezi Mungu, kama sisi wabaya sasa hivi timu inaongoza ligi, ingekuwa wabaya tungekuwa nafasi ya 10, Mungu kamteua awe muheshimiwa na muheshimiwa siku zote hakosei.”

Kwa upande wake Jerry Muri ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amezungumzia juu ya kauli yake aliyosema siku chache zilizopita kuwa wachezaji Moshi ‘Boban’ na Mrisho Ngassa hawapaswi kuitumikia Yanga kwa sasa ”Tatizo kubwa si mwenendo wa Yanga, bali ni kufungwa na Simba hili ndiyo tatizo.

Jerry Muro ameongeza ”Kupoteza mchezo wetu na Simba imemuumiza kila mtu, unajua unaweza ukaongoza ligi lakini kuongoza kwako kukawa hakuna maana kama utafungwa na Simba na ni hivyo hivyo kwa Simba.”

”Hakuna kipimo kikubwa katika vilabu vyetu hivi kwa mwalimu na wachezaji kama utafungwa na Simba au Yanga, mimi kama mwanachama, shabiki na mdau wa soka lazima nafsi itauma.”

”Tunapo cheza na Lipuli, Mbao na kuwafunga, hakuna raha inayokuja kama vile kumfunga Simba, ndiyo tunachangamoto tunakwenda nazo lakini changamoto hizi tukakosa furaha na huo ni mtazamo wangu mimi kama Jerry na siyo kama Mkuu wa Wilaya.”

Hata hivyo Mh Jerry amewaomba radhi wanachama na mashabiki wote wa Yanga waliokerwa na kauli yake dhidi ya mwalimu Zahera, Ngasa paoja na Boban .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents