Ngassa aoa, asimulia darasa la Zola

Ngassa aoa, asimulia darasa la Zola
Mshambuliaji wa Yanga na Taifa Stars, Mrisho Ngassa ameachana na ukapera na amefichua mambo manne ambayo kocha wa timu ya West Ham, Gianfranco Zola alimpa alipokuwa akifanya majaribio ya soka ya
kulipwa

Ngassa aliyeko katika
kikosi cha Stars kinachojiandaa kucheza na DR Congo baadaye mwezi huu
alisema kuwa kocha huyo amempa vitu hivyo ili vimsaidie kukua na kufika
mbele zaidi kisoka, hasa akizingatia kila kitu anachotakiwa mchezaji
yeye anacho.

Alisema kuwa kabla hajaondoka West Ham alikoenda kwa majaribio ya soka
ya kulipwa kwa muda wa wiki mbili, Ngassa alieleza kuwa Zola alimtaka
akiwasili nchini azingatie mazoezi kwa kwenda mara kwa mara kituo cha
mazoezi ya viungo (gym), awe makini na kazi yake ya mpira kwa kujituma
awapo uwanjani.

Pia, Ngassa ambaye alifunga ndoa na LatifabAbdulrahman, Tabata
Kisiwani, Dar es Salaam alisema kocha huyo alimwelekeza awe anafanya
mazoezi kila wakati na kuzingatia na kutii muda na chakula kulingana na
mazoezi anayofanya na gym na hilo litamsaidia kufanya umbo lake dogo
liongezeke.

Pia, alisema kuwa alimwambia kama atachaguliwa katika kikosi cha timu
ya taifa ahakikishe anacheza kwa umakini na kujituma zaidi na aonyeshe
nidhamu ya hali ya juu kwani ndio itakayomfanya aonekane kwa timu
nyingine kwa kuwa timu ya taifa inacheza na timu nyingi za nchi tofauti.

Ngassa alisema ataendelea kuyafanyia kazi hayo mambo kwani anaamini
yatamsaidia kufika mbali na hatimaye ndoto zake za kuwa mchezaji wa
kimataifa kutimia.

Hata hivyo mchezaji huyo anatakiwa kurudi tena nchini humo Julai kwa
ajili ya majaribio ya awamu ya pili baada ya kufuzu ya awali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents