Moto Hauzimwi

Ngoma Africa band yafyatua CD mpya

MK Kundi la “The Ngoma Africa Band” yenye makao yake Ujerumani, wameshitusha ulimwengu kwa kufyatua CD nyingine kwa kasi ya nguvu mpya. CD hiyo iliyobeba jina la “Mama Kimwaga” sugar mum.

Mama KimwagaKasi Mpya!Ari Mpya! usemi na wito wa Rais JK, Usemi huu unafanyiwa kazi katika kila sekta!

Kundi maarufu la “The Ngoma Africa Band” yenye makao yake mjini Oldenburg Ujerumani, wameshitusha ulimwengu kwa kufyatua CD nyingine kwa kasi ya nguvu mpya. CD hiyo iliyobeba jina la “Mama Kimwaga” sugar mum.

CD yao hiyo yenye BONGO DANSI la kukata na shoka himeshapiga hodi katika radio za BBC idhaa ya kiswahili mjini London kwa Bi.Mkubwa, Radio Deutche Welle idhaa ya kiswahili, inayorusha matangazo yake mjini Bonn Ujerumani, ilikuwa inakipiga kibao hiko katika kipindi mahalumu cha utamaduni na sanaa cha tarehe 16/06/2006 alisikika mtangazaji Richard Madete akimhoji mwimbaji na kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Ras Ebby Makunja aka Kichwa Ngumu.Radio nyingine ambayo imepokea kibao hiko ni Radio Voice Of America(VOA) swahili service inayorusha matangazo yake mjini Washington D.C.

Mwimbaji na kiongozi wa bendi hiyo Ras Ebby Makunja alizitaja nyimbo zilizomo katika CD hiyo ni:- Wivu ni Kidonda, Malaika, Jamila, Matembele, Yakibilu, Baba ashibae, Anguruma na Sugar Mum “Mama Kimwaga” nyimbo ambayo imebeba jina la CD hiyo.

Ras Ebby Makunja alisisitiza kwa makampuni na wale wote wataotaka kuwa wasambazaji wa santuri za bendi hiyo wasisite kuwasiliana na meneja wa mauzo wa bendi hiyo kwa anuani hii: [email protected]. Makunja alisema makampuni ya wazawa na wazalendo yatapewa nafasi za mwanzo katika kuzisambaza santuri hizi.

The Ngoma Africa Band ilifyatua Single “RUSHWA NI ADUI WA HAKI” mwanzoni mwa mwezi Mei, wimbo huu umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuteka nyoyo za watu na kuwa kumzo katika kila kona. Mtunzi huyo huyo Ebby Makunja akaja tena na utunzi wa nyimbo saba katika nane zilizomo katika CD yao hii mpya ambapo Mama Kimwaga ana vituko vyake, na pia wimbo wa Baba Ashibae nae anatoa draw kwa vituko vyake.

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW