Burudani

Ngoma mbili za Godzilla anazozitolea macho Bill Nass

Rapper kutoka kwenye Bongo Flava, Bill Nass ametaja ngoma mbili za Bill Nas ambazo anatamani siku moja azifanyie remix.


Bill Nass ambaye amekuwa akihusishwa katika kupotea kwa Godzilla kwenye game, ametaja ngoma hizo kuwa ni Nataka na Kingzilla.

“Nyimbo za Godzilla ambazo natamani kufanya remix ni mbili, ‘Nataka na Kingzilla’, Kingzilla kuna sehemu anasema wanaombea nipata hata supplementary, chuo unajua kuna watu walikuwa wanaombea nipate supplementary au nini, kwa hiyo ni wimbo ambao una mistari ya kunigusa,” ameiambia XXL ya Clouds FM na kuongeza.

“Na ile (mstari) success imerudi kwa potential, me ni boss and still naishi ghetto, yaani boss lakini bado anaishi mtaani. Ni wimbo mzuri ambao alijinadi vizuri na wimbo ambao ni rahisi kwangu kuufanyia remix coz najua mstari baada ya mstari,” amesisitiza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents