Burudani

Ngoma ‘Mziki Majanga” ya Dogo Richy yamfungulia milango ya mafanikio

MwanamUziki Dogo Richy kutoka hapa Kenya, ambaye mpaka sasa bado nyimbo yake ya ‘Mziki Majanga’inaibua joto la hisia mseto kwenye ulingo wa mziki nchini, ameanza kuona green-light katika safari yake ya muziki.

Richy aliwaponda mastaa wengi wa muziki haswaa wale wanaotokea ukanda wa pwani ya Kenya, kwa kuumizwa na uchochole licha ya kupeta kwenye anga za muziki kwa kutoa hits baada ya hits.

Malalamiko haya huenda yamewagusa wadau mbalimbali, wanaoupenda mziki ikiwemo kampuni ya mawasiliano nchini Kenya ya Orange. Wikendi iliyopita, kituo cha redio cha Bahari FM 94.2 Mombasa, kikishirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Orange walifanya road show yao ambayo ilipewa jina ya ‘Market Daya’ na iliwachukua wasanii wawili Susumila (Mmoja aliyetajwa kwenye ngoma #MzikiMajanga) na Dogo Richy ili kutumbuiza katika hafla hiyo ambayo kilele chake ilikua uwanja wa Beach ya Jomo Kenyatta almaarufu kama Pirates uliopo mjini Mombasa.

Dogo Richy akifanya yake katika Road Show ya Bahari FM na Kampuni ya Orange

Wengi wamemfananisha Richy Ree na rapper Controversial wa Bongo Flava Emmanuel Elibariki aka NAy Wa Mitego, ambaye anafahamika kwa weledi wake wakuwachambua na kuwaponda wasanii wenzake wanaofanya Bongo flava bila ya kuogopa.

Si ajabu Dogo Richy ambaye kwa hivi sasa kila kituo cha habari nchini Kenya kinamng’ang’ania kufanya interview na yeye, kupata dili la kuWa ambassador wa kampuni ya Orange. Na kama Orange itafanya hivyo, msanii Richy Ree atakuwa anajiunga na wasanii wenzake ambao wanatia donge nono kwasababu ya kuwa wawakilishi wa mashirika na kampuni hapa Kenya kama rapper Octopizzo ambaye ni ambassador wa shirika lisilokuwa la kiserekali la FILM-AID’S YOUTH MEDIA na King Kaka ambaye mwaka jana 2016 alisaini mkataba (MOU) na chuo kikuu cha ZETECH ambapo rapper huyo anatoa huduma fulani kwa chuo hicho.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Instagram: changez_ndzai
Twitter : ChangezN

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents