BurudaniHabari

Ngoni Kumpa tafu Akon ndani ya Bongo

Ngoni Patrick Nyanzi aka Pato pamoja naye Eddie Mpagi almaarufu kama Ayde E kwa pamoja wanaunda kundi la Ngoni lenye maskani huko Kampala, Uganda.

 

Ngoni

 

 

Story by: Daniel Nyalusi

Patrick Nyanzi aka Pato pamoja naye Eddie Mpagi almaarufu kama Ayde E kwa pamoja wanaunda kundi la Ngoni lenye maskani huko Kampala, Uganda.

Nyimbo yao ya kwanza kabisa ambayo nayo ilikuwa na mahadhi ya RnB “Sekiriba Kya ttaka” ilitoka 1998.

Kundi hilo ambalo linaimarika kadri siku zinavyokwenda limejipatia umaarufu katika siku za karibuni na nyimbo zake za DiGi na NASIIMA GWE ikimaanisha “Tuko Pamoja”.

Wasanii hao wanatumia staili ya muziki wake kama Good Swing (Afro Pop) ambayo inachanganya R n’ B na mirindimo ya Kiafrika kwa kutumia mtindo wa Zouk.

Ngoni wanatarajiwa kuja kutumbuiza jijini Dar es Salaam tarehe 16 ya mwezi huu katika show ambayo itaongozwa nae Gwiji linalo ongoza kwa mauzo kwa wasanii wa Kiafrika nchini Marekani AKON, Ngoni wameshafanya maonesho katika miji mbali mbali Afrika na Ulaya ikiwemo Sweden na Rwanda.

Source: Bongo5

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents