Ngorongoro Run: Race against malaria

Tigo Ngorongoro Run: Race against malaria
Kampuni ya TIGO imejitokeza na kuchangia kiasi cha Dola elfu 10
(10,000) ili kufanikisha mbio za pili za marathon zinazojulikana kama
"Ngorongoro Run : The Race against Malaria", mbio hizo zimeandaliwa na
Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO) ya Minnesota International Health
Volunteers ambao watatumia michango hiyo kwa harakati za kupambana na
ugonjwa hatari wa malari

Katika hafla maalum meneja wa huduma kwa wateja wa Tigo, Innocent Mayawa jana alikabidhi mfano wa hundi ya dola za kimarekani 10,000 kwa Mercy Kimaro mratibu wa shirika hilo, na walioshuhudia ni Irene Kiwia na Nancy Sumari ambao ni wakurugenzi wa Frontline Management kampuni inayoratibu mbio hizo.

Mgeni rasmi katikia mbio za "Ngorongoro Run : The Race against Malaria" atakuwa Dk. Wilbroad Slaa.

Mbio hizo zitafanyika Jumamosi tarehe 18 April, zitaanzia katika geti la kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na kumalizika mjini Karatu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents