Ngozoma Matunda Afariki Dunia

KIONGOZI maarufu wa Klabu ya Yanga, Rashid Ngozoma Matunda amefariki jana katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam alikokimbizwa kwa matibabu baada ya kuugua ghafla.

 

KIONGOZI maarufu wa Klabu ya Yanga, Rashid Ngozoma Matunda amefariki jana katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam alikokimbizwa kwa matibabu baada ya kuugua ghafla.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega aliiambia Mwananchi kuwa wamepata taarifa kutoka kwa ndugu zake kuwa kiongozi huyo mashuhuri aligua ghafla na kukimbiza hospitali, lakini baada ya kufika waliambiwa kuwa amekata roho.
Sisi hatuna taarifa kamili, isipokuwa tunasubiri ndugu watufahamishe nini kimeondoa roho yake baada ya uchunguzi, alisema Madega na kuongeza: ìKikubwa tunasubiri wanandugu wakutane na kutoa taarifa kamili ikiwemo mazishi.
Habari zilizopatikana jana jioni zilieleza kuwa Matunda alikufa kwa shinikizo la damu na mwili wake unatarajiwa kusafirishwa leo kupelekwa Morogoro kwa mazishi.
Matunda amekuwa kati ya viongozi waliokuwa maarufu miaka ya ’90 alivuma zaidi wakati wa mapinduzi ya mara kwa mara ndani ya klabu hiyo pamoja na kuongoza kamati za muda.
Itakumbukwa kuwa Matunda alivuliwa madaraka katika mapinduzi yaliyofanywa na aliyekuwa rais wa kwanza wa Yanga, Tarimba Abbas, Juni 1999 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, IFM na kuzuka mgogoro mkubwa.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents