Soka saa 24!

Ngurumo apokea Sadaka

Twanga_ngurumo_face

BENDI  muziki ya Twanga Pepeta na Msondongoma pamoja na Sikinde wote kwa pamoja wamefanya shoo, kwaajili ya kuchangisha fedha kwaajili ya kumpa kama pongezi mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini Muhidini Ngurumo.

 

Mkurugenzi wa bendi hiyo ya Twanga Pepeta, Asha Baraka amesema kwamba kukusanywa kwa fedha hizo hawamaanishi kwamba wanamsaidia, kwakuwa mwanamuziki huyo hana shida ya kinamna hiyo.

Amesema pia isichukuliwe kwamba mzee huyo anashida sana, ila ni moja ya pongezi kwa kufikisha miaka mingi katika muziki huo, fedha ambazo walifanikiwa kuzipata papo kwa hapo zilifikia takribani laki tatu na nusu, huku zingine akiendeleas kuletewa akiwa stejini.

Twanga_ngurumo_muhidini

Mzee Ngurumo naye alitoa wasahaa yake kwamba, anamshukuru sana Asha Baraka kwa hali aliyoionyesha, kwa muda mfupi tangu aingie kwenye soko la muziki wa dansi Tanzania. Amesema kwamba wapo wasanii wengi na wa muda mrefu lakini wameshindwa kufanya hivyo kama alivyofanya yeye kwa kuonyesha moyo wa kujali wakongwe.

Anasema kwa yeye anamuheshimu sana si kwa hilo la kumchangishia fedha, ila tangu alipoona msaada wake wa kuinua wasanii wa muziki huu na mambo anayoyafanya katika tasnia hii.

Mwisho alisema wapenzi wa muziki wa dansi, wapenzi wa Msondo na wananchi kwa ujumla, watarajie ujio wake mpya hivi karibuni baada ya kupata nafuu kidogo.
Twanga_nguruma_asha

Asha Baraka akiendelea kupokea Sadaka, kwaajili ya mzee Ngurumo.

Twanga_Ngurumo_fedha
Mdau ambaye alikuja kutoa sadaka yake, lakini kasheshe ilikuja pale alipotaka kuchukua kipaza sauti, na kutaka kuongea mawili matatu ambayo yalionyesha wazi yangeleta mgongano wa mawazo na baadae kuzua kasheshe.

Twanga_Ngurumo_Kimobiteli
Wanamiziki wa Twanga, akionyesho Show yao, kuanzia kushoto Dogo Rama, Chaz Baba, na Khadija Kimobitel

twanga_ngurumo_luiza

Twanga_ngurumo_msondo

Mzee Ngurumo baada ya kutoa usia wake, akadondosha bonge la burudani kwa kuchombweza kidogo kidogo

twanga_ngurumo_msondo_pesa

Wakati akichombweza watu wakiendelea kumdondoshea fedha kidogo kidogo.

Twanga_Ngurumo_mwijuma

twanga_ngurumo_tx_junior

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW