Burudani

Ni kweli albamu ya 4:44 ya Jay Z inakaribia kutoka?

By  | 

Baada ya mashabiki kushtushwa na ujio wa albamu mpya ya Jay Z, hatimaye siku ya kuachiwa imefahamika.

Albamu hiyo iliyopewa jina la ‘4:44’ ilizua mjadala mkubwa kwa kuchanganya vichwa vya mashabiki baada ya kuonekana mabango kwenye miji ya New York na Los Angeles yenye jina hilo.

Kwa mujibu wa mtandao wa HipHopDX, umesema albamu hiyo itaachiwa Juni 30 ya mwaka huu kwa mara ya kwanza kupitia mtandao wa Tidal.

Imedaiwa kuwa albamu hiyo itawakutanisha mastaa kama Beyoncé, Damian Marley, Zaytoven, na Swizz Beatz.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments