DStv Inogilee!

Ni kweli nimeachana na Nay wa Mitego – NINI

Msanii Nini ameweka wazi kuwa penzi lake na Nay wa Mitego limefika ukingoni.

Muimbaji huyo amesema ameamua kuachana na Nay wa Mitego kutokana na kumchukulia poa na kuwa na mahusiano na wanawake wengine.

“Ni kweli nimeachana na Nay na niweke hili sawa sijawahi kuishi nyumba moja na Nay na hata hiyo ishu ya wazazi wangu kwenda kwa Nay sio kweli,” amesema.

“Unajua kwenye mahusiano kuna mambo mengi sana na mtu kama mwanaume unaweza ukampenda, ukamuheshimu akawa anakuchukulia poa, anakufanyia drama anakuletea wanawake,” Nini ameiambia Clouds TV.

Utakumbuka mapema mwaka huu Nini alimshirikisha Nay wa Mitego katika wimbo wake unaokwenda kwa jina la Niwe Dawa.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW