Wema Sepetu

Ni kweli nimefunga ndoa – Wema Sepetu (Audio)

Wema Sepetu amefunga ndoa – kwa mujibu wake mwenyewe!

11186959_805536586181319_880415277_n

Akiongea na You Heard ya Clouds FM, Wema aliongea kwa msisitizo kuwa picha alizoweka Instagram juzi zikimuonesha akiwa amevaa shela ni za tukio halisi.

“Never knew what Happiness’ had to offer….. Until now… Im GrateFul & Thankful,” aliandika Wema kwenye moja ya picha hizo na kuwaacha mashabiki wake na maswali kichwani.

“Ilikuwa tu ni harusi ya siri, tumeoana bomani kwasababu yeye ni mkristu, baada ya hapo tukaenda Double Tree. Hatujui tutaenda wapi kwa honeymoon kwasababu I am currently very tight.”

Hata hivyo Wema alikataa kumtaja mwanaume anayedai kumuoa. “Siko tayari kumtaja mume wangu, he is very low profile,” alisema muigizaji huyo.

11202542_1389903921336175_386823191_n

Wema amesema hakutaka kufanya matangazo mengi ya ndoa hayo.

Mrembo huyo amedai kuwa hata miezi miwili haijafika tangu wafahamiane na mwanaume huyo. “I need a husband, I need a person ambaye ntasettle naye, nimekaa peke yangu muda mrefu.”

Unaamini Wema ameolewa kweli?

Msikilize hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents