Habari

Ni lini Serikali itaanza kutambua kazi zinazofanywa na tasnia ya habari? (+Video)

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa,Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha wanahabari kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na kanuni na taratibu ili kulinda amani na utulivu katika nchi.


Naibu Waziri wa Habari, Sanaa,Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura

Hayo yamezungumzwa na Naibu Wambura, Leo hii Mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge, Devotha Minja mbunge wa viti maalum liliuliza,

“Waandishi wa habari wanafanyakazi nzuri katika kuelimisha jamii, Je, ni lini Serikali itaanzisha mfumo utakaotambua kazi zinazofanywa na tasnia ya habari?

“Serikali inatambua na kuthamini sana kazi zinazofanywa na vyombo vya habari nchini, mchango wa tasnia ya habari ni mkubwa katika kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii, kwa kutambua mchango huo serikali imeruhusu kuwepo kwa vyombo vya habari vya umma na sekta binafsi yakiwemo Makampuni binafsi, mashirika ya kidini na kijamii,” alisema alisema Wambura.

“Aidha mchango wa vyombo vya habari una toka na sera, sheria, mipango na taratibu zilizowekwa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania mfumo unaotambua kazi ya tasnia ya habari nchi uko tayari katika kudhihirisha hilo, Serikali ilitunga sera ya habari na utangazaji ya mwaka 2003, sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, na sasa ina sheria na huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2017.”

“Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha wanahabari kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na kanuni na taratibu ili kulinda amani na utulivu katika nchi yetu,” alifafanua.

Video:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents